Watalii duniani wajipanga kuja Tanzania kushuhudia kupatwa kwa jua September 1, 2016!


Tanzania itapokea wageni wengi kutoka mataifa ya nje kuanzia mwishoni mwa mwezi August mwakani watakaokuja kushuhudia kupatwa kwa jua (annular eclipse) kutakakotokea September 1, 2016.


Annular eclipse hutokea pale jua na mwezi zinapokuwa kwenye mstari mmoja lakini umbo la mwezi ni dogo zaidi kuliko la jua na hivyo jua huonekana kama ringi inayong’aa sana au kitu cha duara kinachoizunguka duara nyeusi ya mwezi.

Kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Atlantic, kutaenda Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji na Madagascar na kisha kwenye bahari ya Hindi.

Wataalam wanadai kuwa Tanzania ndio itakuwa sehemu ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema zaidi na kuvutia watalii wengi kutokana na kile mtandao wa Independent wa Uingereza unasema ni “dependable weather, invariably clear “big skies”, abundant wildlife and peaceful reputation make it a top tourist destination.”

Maeneo yatakayoona vizuri tukio zima litakalochukua dakika tatu hadi sita ni kwenye maeneo ya Mbeya na Tunduru. Maeneo mengine ya Tanzania yatashuhudia tukio nusu.

Tayari makampuni ya safaris yameshapanga ratiba ya safari za kuja kwenye tukio hilo linalotokea kwa nadra sana.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment