Marekani yatoa silaha kwa waasi Syria





wapiganaji wa kikurdi, wanaoungwa mkono na waasi wa kiarabu, wamefanyikiwa kuwaondoa wanamgambo wa IS katika maeneo mengi ya Syria.

Jeshi la Marekani limetoa zaidi ya tani 45 za silaha kwa waasi wanaopambana na wanamgambo wa Islamic State (IS) kaskazini mashariki mwa Syria.

Jeshi hilo liliangusha shehena ya vifaa katika jimbo la Hassakeh, Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Marekani ameeleza.

Shehena hizo zimeripotiwa kuhusisha silaha ndogo ndogo,kubwa na maguruneti.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Marekani kuacha mpango wa gharama ya dola za marekani milioni mia tano wa kuwafundisha maelfu ya waasi kupambana na IS

Badala yake imeelezwa kuwa fedha hizo zitatumika kugharimia silaha ambazo zitakuwa zinahitajika kwa makamanda wa makundi ya waasi ambao wako katika maeneo ya mapambano.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

1 comments: