Nicki Minaj apanga kukusanya tuzo 2016








MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, amesema kuwa mwaka 2016 atahakikisha anajikusanyia tuzo mbalimbali.

Mwanadada huyo ambaye bado anatamba na wimbo wake wa ‘Right to my side’, amesema mwaka huu amechukua tuzo mbalimbali lakini 2016 atahakikisha anaongeza idadi ya tuzo.

“Tunaumaliza mwaka 2015, nimefanikiwa kuchukua tuzo mbalimbali na sasa nimejipanga kwa ajili ya mwaka 2016 ambapo nitahakikisha najikusanyia tuzo nyingi zaidi ya 2015.

“Maandalizi nimeyaanza tangu mwaka huu kwa kuwa ninajua ushindani uliopo katika muziki wa hip hop, ninaamini nitafanikiwa kutokana na ushirikiano ninaopata kutoka kwa mpenzi wangu Meek Mill,” alisema Minaj.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment