Trey Song kufanya ‘colabo’ na Wizkid, Davido






NYOTA wa muziki nchini Marekani, Tremaine Neverson ‘Trey Song’, amesema yupo tayari kufanya kazi na mkali wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid.

Msanii huyo ambaye alikuwa nchini humo wiki iliyopita kwa ajili ya kufanya shoo kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismasi, amesema amekuwa akivutiwa na wasanii wa Nigeria, hivyo yupo tayari kufanya nao kazi huku akitarajia kufanya na Wizkid.

“Afrika kuna wasanii wengi ambao wana uwezo wa kufanya muziki wa hali ya juu, tayari nimefanya kazi na Davido na natarajia kufanya na Wizkid.

“Ninaamini hawa ni wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa nchini Nigeria, ila kuna wengi wenye uwezo mkubwa,” aliandika Trey Song kwenye akaunti yake ya Instagram.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment