Faith Evans ana imani kesi ya mauaji ya Notorious B.I.G itafunguliwa tena



Faith Evans amedai anaamini kuwa siku moja kesi ya mauaji ya rapper Notorious B.I.G itafunguliwa tena.


Muimbaji huyo aliyeolewa na emcee huyo mzaliwa wa Brooklyn, ametaka kuwepo na msisitizo zaidi katika masuala ambayo hayakupatiwa majibu.

“Tunachoweza kufanya ni kuwa na imani kuwa hiyo itatokea,” Faith aliuambia mtandao wa The Huffington Post alipoulizwa kuhusu Biggie.

“Lakini tuna furaha tu kuwa tupo hapa kuitunza heshima yake na kuhakikisha kuwa watoto wake wana furaha na wanaishi maisha mazuri.”

Muimbaji huyo pia alidai kuwa polisi wa Los Angeles wanajua ni nani aliyempiga risasi marehemu mume wake ila hawataki kumtaja hadharani.

“Tunajua aliuawa, lakini tunaamini kuwa LAPD wanamjua nani aliyehusika. Hichi ndicho tunachoamini.”

The Notorious B.I.G. aliuawa mwaka 1997 jijini Los Angeles.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment