Kanye West aruhusiwa kutoka hospitali


Kanye West ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa kwa zaidi ya wiki moja.



Baada ya kuwa katika uangalizi wa afya yake katika hospitali ya UCLA Medical Center, rapper huyo sasa amerejea nyumbani na mke wake Kim Kardashian kuungana na watoto wao, North na Saint.

West atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wake, Michael Farzam. Huyu ndite daktari aliyepiga simu ya 911 siku ambayo West alipelekwa hospitali, Nov. 21.

Rapper huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili yaliyochangiwa na uchovu, ukosefu wa usingizi na upungufu wa maji mwilini. Matatizo hayo yalipelekea kusitishwa kwa ziara yake ya Saint Pablo.

Matatizo mengine yanayomsumbua rapper huyo ni msongo mkubwa wa mawazo, wasiwasi na huzuni ya kifo cha mama yake. Bado ataendelea na matibabu ya kisaikolojia na ya kawaida.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment