Kasi ya ‘Hapa Kazi Tu’ yamtengua Mkurugenzi wa TIC



Rais Magufuli amemtengua Mkurugenzivwa TIC, Juliet Kairuki baada ya kushindwa kuchukuwa mshahara wa serikali takribani kwa miaka mitatu.



Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda alitoa taarifa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais Magufuli kupata taarifa kuwa mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiliwa mwaka 2013 hatua ambayo imezua maswali mengi kwa rais Magufuli.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo Bi. Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya awamu ya tano atapangiwa kazi nyingine huku mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya atakaye kiongoza kituo hicho cha uwekezaji umeshaanza.

Aidha kwenye taarifa ya Prof. Mkenda amesema Bw. Clifford Katondo Tandali, ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC.

Credit bongo5
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment