TID afunguka kuwahi kuwa kimapenzi na Wema, na walivyo achana akawa 'player'






Msanii mkongwe wa muziki, TID amesema kipindi cha nyuma alikuwa anatoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu lakini baadae alitemwa hali ambayo ilimuumiza sana. Akizungumza katika kipindi cha Clouds TV Ijumaa hii, TID amesema hali hiyo ilimfanya atoke na wasichana wengi.

“Nilikuwa ‘namdate’ Wema Sepetu akaniambia sikutaaki, tangu kipindi hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikitokea Wema anataka kurudi hakuna nafasi, I’m occupied,” alisema TID.

TID amesema katika kipindi hicho aliumizwa sana na jinsi magazeti yalivyokuwa yanamuandika vibaya.

“Wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo lakini wamagazeti walizichukua picha na kufanya yao, it was bad. Mimi nikasema sawa lakini niliumia sana,” alisema TID. Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Confidence’ aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na Dully Sykes.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment