Bifu la Diamond na Alikiba Limeisha? Meneja wa Diamond Apiga Picha ya Pamoja na Alikiba



Kitu ambacho mashabiki wengi wa Music Tanzania na hata nje ya Nchi wangependa kusikia kinaweza kikawa kimekaribia, Meneja wa Diamond, Salaam amepiga picha ya Pamoja na mpinzani mkubwa wa msanii wake, Alikiba.

Haijajulikana nini kinaendelea lakini inawezekana labda ugomvi wa wasanii hao wawili umefikia mwisho na labda tutegemee chochote kutoka kwa hao wasanii wawili. Kweli mbongo mpe picha story ataandika mwenyewe


Picha hiyo inaonekana imepigwa jana, ukiangalia vizuri kwenye hiyo picha utamwona Ne-yo kwa nyuma, Kwahiyo iko wazi kuwa meneja wa Diamond yupo Kenya pamoja na Alikiba. Kitu kingine cha kutegemea ni collabo ya Diamond na Ne-yo, Diamond alikutana na Ne-yo mwezi uliopita Afrika kusini na aliahidi kuwa kuna kitu kinafata kwahiyo inawezekana meneja wa Diamond yupo Nairobi kwa ajili ya kukamilisha collabo hiyo.

Alikiba ameenda jijini humo kwa ajili ya Coke Studio ambapo pia ataungana na wasanii wengine wa Afrika kushirikiana na Msanii wa Marekani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment