Lowassa Amtuhumu Rais Jakaya Kikwete Kwa Kuuharibu Uchumi wa Tanzania...... Asema Vitu vimepandishwa na Tembo Wanauawa Hovyo


EDWARD Lowassa, mgombea urais wa Chadema amesema, Rais Jakaya Kikwete ameharibu uchumi wa Tanzania.

Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho jana mchana, Lowassa alisema;

“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”

“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”

Aidha Lowassa alisema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.

“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.

“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” alisema Lowassa.


 Angalia video hii hapo chini  umsikie  Lowassa  akitoa  tuhuma  hizi.:-

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment