Mo Music kuachia single mpya ‘Skendo’ kwenye birthday yake Nov.14
Msanii aliyewashtua mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva kwa single yake ya kwanza ‘Basi Nenda’ mwaka jana, ambayo ilikuja kuwa kama ‘wimbo wa taifa’ kwa jinsi ilivyokubalika, Mo Music anarudi na single mpya iitwayo ‘Skendo’.
Novemba 14 ni birthday ya mwimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Moshi Katemi kutoka Mwanza, na ndio ameichagua kuwa siku ya kuiachia single hiyo ya tano baada ya ‘Nitazoea’.
‘Skendo’ imeandikwa na kutayarishwa na producer Lollipop ambaye ndiye aliyehusika na uandishi wa nyimbo zilizopita za Mo Music.
Hivi karibuni Mo Music aliiambia Bongo5 kuwa yeye na uongozi wake wanajipanga kufanya mazungumzo na mwigizaji wa filamu Elizabeth “Lulu” Michael ili awe video model kwenye video yake mpya.
0 comments:
Post a Comment