Polisi 'wavamia' washukiwa na mashambulio Paris






Maafisa walizingira sehemu ya mtaa wa Saint Denis wakisaka washukiwa wa mashambulio ya Ijumaa

Washukiwa wawili wamefariki baada ya maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini mwa Paris, wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.

Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea mapema asubuhi kwenye mtaa huo. Operesheni hiyo inadaiwa kumlenga mwanamgambo wa Islamic State Abdelhamid Abaaoud ambaye amedaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129.

Maafisa kadha wa polisi wamejeruhiwa kwenye operesheni hiyo, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.


Afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa, mwandishi wa BBC James Longman

Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.

Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".
Moja kwa Moja: Operesheni Saint Denis



Polisi wamewaondoa raia kutoka eneo hilo

Awali, duru za kiusalama zilisema video ya kiusalama ilikuwa imeonyesha huenda kulikuwa na mshambuliaji wa tisa mashambulio hayo ya Ijumaa.

Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.

Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.

Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.



Eneo ambalo polisi wameshambulia ni karibu na uwanja Stade de France ambako milipuko ilitokea Novemba 13.

Uwanja wa taifa wa michezo wa Stade de France, ambako washambuliaji walilipua mabomu Ijumaa, umo kwenye mtaa huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment