Ushauri wa David Beckham kwa mchezaji Memphis Depay kuhusu Jezi namba 7



Jezi namba 7 ni miongoni mwa jezi zenye heshima kubwa katika klabu ya Manchester United na moja kati ya watu walioipatia heshima jezi hiyo ni David Beckham na Cristiano Ronaldo.



Memphis Depay aliyesajiliwa msimu huu na klabu ya Manchester United akitokea PSV Endhoven ya Uholanzi kwa dau la pound milioni 25 ambaye ndo anavaa jezi hiyo kwa sasa.

Depay ambaye kwa wiki za karibuni amekuwa akikaa benchi na mchezaji Jesse Lingard kuchukua nafasi yake, inatajwa kuwa na presha kubwa kutokana na wengi kutaka kuona anaifanyia makubwa jezi namba 7 kama walivyofanya Cristiano Ronaldo na David Beckham.

David Beckham amempa ushauri Memphis Depay kuwa hatakiwi kuwa na presha au kuogopa kuvaa jezi hiyo licha ya kuwa inatajwa kuwa na mafanikio makubwa Man United lakini ni heshima kwake kuvaa jezi namba saba.



“Sioni kama jezi namba 7 inatisha au kuogopesha chochote mimi nafikiria ni heshima kuivaa, unapopewa jezi namba 7 haina maana ya kwamba hadi uwe umeshinda au huyo mchezaji awe amepata mafanikio sana, lakini mwisho wa siku ni jezi maalum kuivaa ila sifikirii kama inakuwa na presha kuivaa binafsi ni jezi inayonihamasisha uwanjani” >>> Beckham

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment