Watu wenye silaha washambulia hoteli Mali





Polisi wa Mali wameingia katika hoteli hiyo

Wanajeshi wameingia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako baada ya watu wenye silaha kuishambulia na kushikilia watu mateka.

Uvamizi huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa asubuhi kwenye hoteli hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.

Ripoti za karibuni zaidi zinasema mateka 80 wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na Wamarekani.

Awali, kampuni inayomiliki hoteli hiyo Rezidor Hotel Group ilikuwamesema watu 170 walikuwa wameshikiliwa mateka na "watu wawili".

Radisson Blu HotelImage captionTovuti ya hoteli hiyo inaieleza kama "hoteli ya kifahari"

Baadhi ya ripoti zinasema watu walioshambulia hoteli hiyo huenda wakafika 10.

Milio ya risasi inasikika kutoka nje ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, shirika la habari la AFP linasema.

Mwandishi wa BBC Afrique Abdourahmane Dia anasema hoteli hiyo, inayomilikiwa na Wamarekani, hutumiwa sana na raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Mali.
Moja kwa Moja: Shambulio hotelini Bamako

Ufaransa ambayo imekuwa na wanajeshi Mali tangu 2013 inaripotiwa kutuma wanajeshi wake kusaidiana na wanajeshi wa Mali. Aidha, polisi maalum wapatao 50 wametumwa kutoka Paris.

Rais wa Mali aliyekuwa ziarani Chad amekatiza safari yake na anatarajiwa kurejea Mali wakati wowote.

Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13, wakiwemo wafanyakazi watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu katika mji wa Sevare, katikati mwa Mali.

Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na familia.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment