Louis van Gaal: Rashford ana kila kitu anachostahili kuwa nacho mshambuliaji mahiri


Kocha Louis van Gaal amekiri kuwa kinda wa Machester United Marcus Rashford ana kila kitu anachostahili kuwa nacho mshambuliaji mahiri.



Louis van Gaal ameyasema hayo baada ya mechi na mahasimu wao City baada ya kinda huyo kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi wa 1-0.



Bao la dakika ya 16 la Rashford lilitosha kuipa ushindi United na kupunguza pengo la pointi kwenye Premier League kati yake na City ambapo sasa Manchester United imeachwa kwa pointi moja tu.

Van Gaal akakiri kuwa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 alijihakikishia namba mara tu alipomchezesha mchezo wake wa kwanza mwezi uliopita. Hadi sasa Rashford amesha funga mabao matano katika michezo nane aliyocheza


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment