Joe Hart na Raheem Sterling watakuwa nje kwa mwezi mmoja


Wachezaji wa klabu ya Manchester City Joe Hart na Raheem Sterling watakosa mechi za kirafiki za England dhidi ya Germany na Holland baada ya nyota hao wawili kuumia na kutolewa katika mchezo wao na Manchester United.
3265D7DE00000578-3501598-image-a-60_1458495421745
Joe Hart aliumia mguu wake wa kulia katika harakati za kumuwahi Anthony Martial asifunge baada ya pasi mbovu ya nyuma kutoka kwa beki Martin Demichelis na Sterling alitolewa kipindi cha kwanza baada ya kugongana na Juan Mata.
326595A000000578-3501598-image-a-1_1458500190048
Kwa mujibu wa kocha wa City, Manuel Pellegrini amesema nyota hao watakuwa nje kwa mwezi mmoja na kukosa mechi za maandalizi ya Timu ya Taifa kwaajili ya Euro 2016, ambapo England itajipima nguvu na Ujerumani huko Berlin Jumamosi ijayo kabla ya kurejea Wembley kuikabili Holland siku tatu baadae.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment