Fid Q afikiria kutilia maanani uongozaji video, ni baada ya kupongezwa kwa mawazo yake kwenye video mpya ya Ben Pol



Fid Q anafikiria kuweka nguvu zaidi kwenye uongozaji wa video za muziki baada ya hivi karibuni kupongezwa kwa ubunifu aliouonesha kwenye video ya wimbo mpya wa Ben Pol, Moyo Mashine.



Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, rapper huyo alisema Moyo Mashine inakuwa video ya pili kuitengenezea wazo la video baada ya ile ya wimbo wake ‘Walk It Off.’

Alisema Ben Pol alimtumia nyimbo kadhaa ukiwemo Moyo Mashine ili ampe ushauri upi wa kuutoa lakini baada ya kuusikia wimbo huo anasema alipata hadi wazo la video yake.

“Nikamtumia picha na maandishi kwamba nataka hii picha ikae hivi, uvae hivi. Kwahiyo sijadirect tu, ni mpaka kudesign mavazi na vitu kama hivyo,” alisema Fid.

Rapper huyo amesema ataongoza video zingine kibao zijazo na kwamba anawashukuru mashabiki wa muziki kwa kukubali kazi ya Ben Pol.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment