Exclusive: Ben Pol Afunguka Jinsi Mama Yake Alivyo Teseka Wakati Baba Yake Alivyo Fungwa Akiwa Tumboni




Msanii Ben Pol ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Moyo Mashine' amefunguka na kusema kuwa Baba yake mzazi alifungwa kifungo cha miaka miwili wakati mama yake mzazi akiwa na ujauzito wake.

Ben Pol amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt kinachorushwa na EATV na kudai kuwa licha ya baba yake kufungwa lakini Mama yake mzazi alipigana mwanzo mwisho kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka alipozaliwa na kumpa malezi.

"Unajua mimi najua nilipotoka mpaka nilipofika hapa naweza kusema I made it, wakati mama yangu ana ujauzito wangu wa miezi sita baba yangu mzazi alifungwa jela miaka miwili hivyo mama alipambana kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka nazaliwa na kunilea hivyo leo kwa hapa nilipofika huwa napenda kushare historia yangu ili watu wajue," alisema Ben Pol.

Mbali na hilo Ben Pol anasema kuwa yeye hakuzaliwa hospitali bali mama yake mzazi wakati wa kumzaa yeye alijifungua akiwa nyumbani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment