Mr Blue kuja na ‘Mboga Saba’ aliyomshirikisha Alikiba


Nina uhakika hata kama bado sijaisikia, hii inaqualify kuwa moja ya collabo zitakazozungumziwa zaidi mwaka huu.



Mr Blue ameinspire wasanii wengi sana wanaofanya vizuri sasa hivi. Ni rapper aliyefanikiwa akiwa na umri mdogo kupitia hits zake kama ‘Blue Blue’ na ‘Mapozi.’

Na pale anapoamua kumshirikisha staa wa muziki mwenye fan base kubwa mno kwenye muziki wa bongo, Alikiba, uhakika wa kuzalishwa hit hauepukiki.

Nimekuwa nikifahamu ujio wa wimbo wa Kabayser aliomshirikisha Kiba lakini wikiendi iliyomalizika ndipo nimefahamu pia jina la collabo yao. Wimbo unaitwa ‘Mboga Saba’ na umetayarishwa na mshindi wa mara kibao wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava, Man Walter.

Blue na Alikiba wote wana historia nzuri ya kufanya hit na Man Walter.Tabasamu ya Mr Blue na Mwana ya Alikiba zote zilitayarishwa na producer huyo wa Combination Sounds. Tunaingoja kwa hamu ‘Mboga Saba.’




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment