Utafiti: Pombe ni chanzo cha ugonjwa wa saratani


Watafiti wa afya kupitia jarida la Addiction wamedai kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya unywaji wa pombe na aina saba za saratani.


Aidha wataalamu hao wamegundua kuwa saratani ambazo imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana, saratani ya matumbo na saratani ya matiti.

Aidha mwezi Januari mwaka huu, afisa mkuu wa afya kutoka nchini Uingereza alitoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kwa kiwango chochote kile kina madhara ndani ya mwili.

Mpaka sasa watu zaidi ya laki tano wanakadiriwa kufa kutokan ana ugonjwa wa saratani kwa mwaka 2012 pekee. Hata hivyo mpaka sasa bado haijabainika kibaiolojia uhusiano wa pombe na saratani inatokeaje.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment