Rapa Young Dee
Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amedai wimbo wake mpya aliouachia ‘Bongo Bahati Mbaya’ siyo ujio wake rasmi ambapo amedai ni kama alikuwa anafanya sound check kabla ya show kamili.
Rapa huyo ameiambia Bongo5 kuwa studio ana project nyingi kali ambazo zinasubiria muda wake wa kuingia sokoni.
“Kutoka King Cash mimi ndio msanii wa kwanza na kuna project nyingi kali zinakuja hii ‘Bongo Bahati Mbaya’ ni kama nilikuwa nafanya Sound Check, show kamili inakuja,” alisema Young Dee. “Mashabiki wanamjua Young Dee ni nani, kwahiyo mimi naomba wakae mkao wa kula kuna mambo makubwa sana nimefanya na Mr Ttouch, tena ni hatari,”
Rapa huyo ambaye zamani alikuwa chini ya label ya Millian Dollar Boys (MDB) ya Max Rioba, amedai anaimani label yake mpya King Cash itamfanyia mambo makubwa katika muziki wake.
Source Bongo5.
0 comments:
Post a Comment