Dogo Janja kuchafua mtaa na ‘Ukivaaje Unapendeza?’



Msanii wa muziki wa hip hop, Dogo Janja baada ya kujinadi kuwa ni mkali wa kuvaa Bongo na baadaye kupingwa na baadhi ya wadau, rapa huyo anajipanga kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Ukivaaje Unapendeza?.


Rapa huyo ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kufanya project hiyo baada ya kuona watu wengi wanauzungumzia muonekano wake wa mavazi.

“Suala la muonekano wangu wa mavazi limekuwa gumzo kusema kweli, watu wananiangalia sana, wengine wanasema vibaya,” alisema Janjaro. “Kwa hiyo nimeona nifanye project mpya ‘Ukivaaje Unapendeza?’ halafu tuone mambo yatakuwaje,”

Project hiyo ambayo imetayarishwa katika studio ya MJ Record chini ya producer, Daxo Chali akishirikiana na Marco Chali, itatoka muda wowote kuanzia sasa.

Rapa huyo kwa sasa bado anaendelea kufanya vizuri na project yake iliyopita, Kidebe.

Source Bongo5

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment