Samsung kuingiza simu mpya sokoni baada ya kufeli kwa Galaxy Note 7



Baada ya Samsung kulazimika kusitisha utengenezaji wa simu za Galaxy Note 7 kutokana na tatizo lake la kulipuka, kampuni hiyo imeamua kuja na simu mpya ya Galaxy Note Fan Edition.



Muonekano wa simu mpya za alaxy Note Fan Edition
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imedai, utengenezwaji wa simu hizo umetokana na baadhi ya vitu kutoka katika simu ya Galaxy Note 7 ambayo ilisitishwa kuingia sokoni tangu mwezi septemba mwaka jana kutokana na kuleta madhara kwa baadhi ya watumiaji kutokana na mlipuko kwenye simu hizo.

Taarifa imeendelea kwa kusema simu hizo mpya zitaanza kuuzwa Julai 7 mwaka huu nchini Korea Kusini ambapo ndipo yalipo makao makuu ya kampuni hiyo.



Picha ya simu za Galaxy Note 7 ambazo zilisitishwa kutengenezwa kutokana na kulipuka

Simu za Galaxy Note 7 zilikadiriwa kuuza kiasi cha dola bilioni 5.3 duniani kote ikiwa ni muda mfupi tangu ziingie sokoni lakini baada ya kusitishwa kwa uuzwaji wake inadaiwa kampuni hiyo ilipata hasara ya takribani dola bilioni 10.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment