Bushoke aitaja sababu inayompa kiburi kutohaha kuachia kazi mpya




Muimbaji wa nyimbo zilizowahi kuhit zikiwemo ‘Mume Bwege’ na ‘Msela Jela’, Bushoke amesema licha ya kutokuwa na kazi mpya bado anajiamini kuwa show zake zina mapya mengi.



Bushoke akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Mlimani City wiki iliyopita ambapo alitumbuiza kiasi cha Rais kumwita na kumpongeza
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Bushoke alisema bado anaamini nafasi yake ipo.

“Nashukuru Mungu siku zote huwa nategemea kufanya vitu vizuri japo kazi zangu nyingi nimefanya zamani, ila napopata nafasi nzuri, steji nzuri na wapigaji wazuri huwa nafanya kitu kizuri haijalishi nyimbo nimezifanya lini. Kama mlivyoona pale niliimba wimbo wa ‘Mume Bwege’ ambao niliimba kitambo ila pale niliibadili kabisa na kuifanya kuwa mpya ndio maana watu waliweza kufurahi,” alisema Bushoke.

Bushoke amewataka wasanii wengine pia kujiimarisha katika performance za live.

“Kwa hapa nyumbani wasanii wanaimba vizuri ila performance zao sio live, wanapaswa kutambua tu muziki mzuri ni live Performance. Hivyo wasanii wenzangu wanapaswa kutumia muda wao mwingi katika kuboresha kazi zao ili waweze kufanya performance nzuri zaidi, maana hiyo ndio inaweza kuwa tiketi kwa msanii kufanya vizuri na kuweza kufika mbali zaidi katika kazi,” alishauri Bushoke.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment