Rockstar4000 watangaza ujio wa collabo ya Alikiba na Ne-Yo


Kampuni inayomsimamia Alikiba, Rockstar4000 imetangaza kuwa msanii huyo atamshirikisha msanii wa Marekani, Ne-Yo.

page

Imetoa tangazo hilo kupitia Instagram.
“Exciting News: African superstar Alikiba will be collaborating with International Superstar Ne-Yo — More news to follow…. #kingkiba #ROCKSTAR4000,” imeandika.
Ne-Yo ambaye alitumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu, anatarajia kuja tena Afrika hivi karibuni ambapo ataungana na wasanii waliopo kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika jijini Nairobi, Kenya.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii waliopo kwenye msimu huo mpya.
Album mpya ya Ne-Yo Non-Fiction ilifika namba moja kwenye chati ya Billboard’s Top R&B/Hip-Hop Albums.
Pamoja na Ne-Yo, Alikiba pia anatarajia kumshirikisha msanii wa Nigeria, Davido.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment