Chamber Squad yajipanga kuachia kazi mpya




Rapper Noorah amesema kundi lake la Chamber Squad lipo mbioni kuachia kazi mpya.












Akizungumza na E-Newz ya EATV jana, Noorah alisema tayari ameshaandaa kazi mpya za kundi hilo na wanachosubiria ni kumalizika kwa uchaguzi.

“Kazi zitatoka, kuna kazi ya Chamber nzima ambayo ipo tayari, lakini kwa sasa hivi kutokana na timing za kibiashara hatutazitoa sasa hivi, mpaka hizi vurugu vurugu za uchaguzi zipite kwanza,” alisema.

“Kazi zangu mwenyewe zipo, kuna ngoma mbili nilishafanya, zenyewe zipo kwenye foleni kazi zilikuwa zimeshafanyika lakini kuna mambo yameingilia. So far sina mtu yoyote wa kunisimamia, I real need a management. Watu ambao wako tayari kufanya kazi, na muda wao wote wanauweka kwenye kazi hii,” aliongeza Noorah.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment