Christian Bella anataka mwanae acheze soka la Ulaya





Christian Bella amesema anajipanga kumpeleka mtoto wake wa kiume kwenye shule za mpira nchini Sweden.

Bella ameiambia Bongo5 kuwa anajisikia fahari kumchagulia mwanae kwenda kwenye shule za mpira kwa kudai mchezo huo unalipa sana kwa nchi za Ulaya.

Unajua mzazi ndio mtu pekee anayeweza kumpeleka mtoto wake sehemu salama,” amesema muimbaji huyo. “Ndio maana mimi nikaona nikimpeleka mwanangu kwenye shule za kucheza mpira nitakuwa nimemsaidia sana. Mpira unalipa sana Ulaya.

Unajua baba yake ni mwanamuziki na naamini pale alipo ndani yake ana chembechembe za muziki, lakini nikaona tu nimtafutie kitu kingine ambacho pia kinaweza kuwa bora,” aliongeza.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment