Hamisa Mobeto ahoji, Hadi lini tutavaa mawig ya kichina na nguo za Kimarekani?












Mwanamitindo Hamisa Mobeto amesikitishwa na Tanzania kuendelea kuwa nchi isiyojiweza kiviwanda licha ya kuwa na rasilimali na nguvu kazi ya kutosha.
Akizungumza jana kwenye ukumbi wa New Africa Hotel katika mdahalo uliopewa jina ‘Ndoto Kubwa’ ulioandaliwa na Tanzania Initiative kwendana na kilele cha siku ya vijana duniani, Mobeto alisema anachukizwa na wasichana kutegemea urembo kutoka China, Marekani na nchi zingine.

“Inasikitisha mimi kila kitu ninachovaa nguo kutoka nchini nyingine, ili nionekane lazima nivae nywele kama mchina, nivae nguo kama mmarekani, viatu sijui kama mtu gani,” alisema Mobeto.

“Sisi tunaamini Tanzania tuna maeneo mengi sana ambayo hayajatumika. Serikali ina uwezo wa kujenga kiwanda cha kutengeneza nguo, ambapo sisi kama sisi tunaweza kuvaa vitu ambavyo vinatoka kwetu, ambapo tuwe proud kwamba nchi yetu tunavaa vazi letu hili linatoka Tanzania,” aliongeza.

“Inasikitisha sana kuona mmasai amekaa Magomeni sehemu fulani barabarani anatengeneza viatu vya kimasai lakini nchina amekuja anatengeneza hivyo hivyo viatu vya kichina ambavyo ni fake na watanzania wanavinunua na kuvivaa wakati tungeweza kumwezesha yule mmasai wetu ambaye amekaa chini na kupigwa na jua kwa kutengeza bidhaa bora.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment