Hemedy PHD kuja na video ya wimbo aliotaja majina ya ‘mademu’ wake wote aliowahi kuwa nao!


Msanii mwenye a.k.a ndefu kuliko wote Tanzania, Hemedy PHD anatarajia kuwaweka hadharani kwa kuwataja majina warembo wote aliowahi kudate nao.


Hemedy ambaye ameachia video mpya “Imebaki Story” wiki iliyopita, amesema kuwa tayari ana video nyingine kibindoni, ya wimbo uitwao “Pappy Why Are You So Fly”.

“Nyingine inakuja Sepetember 30 kuna video yangu mpya inakuja nimesha shoot iko kapuni, inaitwa “Pappy Why Are You So Fly”. Alisema Hemedy kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Ameongeza kuwa katika wimbo huo ameimba kuhusu wasichana aliowahi kuwa nao kimapenzi, na amewataja kwa majina kuanzia mwanzo hadi mwisho wa wimbo huo wenye karibia dakika nne.

Humo ndani nimejaribu kumention mademu zangu wooote mbao nimeshawahi kuwa nao mpaka kufika hapa kwahiyo ni bonge moja la hit. Siku hizi unajua nimetulia nina mwanamke mmoja kwahiyo nikianza kuji proud kuwataja itaniletea kidogo tatizo, but all in all wote nimewataja. Jiulize nyimbo ina dakika 3 na sekunde 50 nataja majina tu jiulize je mangapi?”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment