Jeshi la Polisi Lakanusha Kupiga Marufuku Maandamano ya Kumsindikiza Kuchukua fomu Mgombea urais Chadema,Edward Lowassa



Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amekanusha kupiga marufuku maandamano ya kumsindikiza Lowassa Kuchukua fomu ya kugombea urais ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi.

Kova amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayo anzia ofisi za CHADEMA kwenda NEC,lakini ya kutoka Nec kwenda makao makuu ya CUF Buguruni hawayatambui.

Katika Hatua nyingine, Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe amesema hawana taarifa yoyote ya zuio la maandamano toka jeshi la polisi.

Mbowe amesisitiza kuwa maandamano ya kumsindikiza Lowassa NEC yako palepale na amewataka wapenzi na wafuasi wa UKAWA wasiogope.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment