Karibu watu 60 wauawa Nigeria


Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchini lililoendeshwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram



Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa ukweli kuwa ilichukua siku tano kabla ya shambulizi hilo kujulikana, ni ishara kuhusu jinsi hali ya usalama ilivyo eneo hilo

Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi

Mikakati ya jeshi Nigeria imelidhoofisha kundi la Boko Haram miezi ya hivi majuzi lakini sehemu zingine za kaskazini mashariki mwa Nigeria kama Yobe na jimbo jirani la Borno yako katika hali mbaya kiusalama
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment