Mr Blue amefunguka kuwa ni wakati wake kutoka kimuziki, baada ya kukaa kimya takribani kwa miaka mitatu


Msanii Khery Sameer Rajab maarufu kama Mr Blue amefunguka na kusema sasa ni wakati wake kutoka kimuziki na kazi mpya baada ya kukaa kimya takribani kwa miaka mitatu tangu alipoachia wimbo wake ambao uitwao 'Pesa'.


Mr Blue kupitia katika mtandao wa Instagram amewashukuru mashabiki wake kwa uvumilivu wao vile ambavyo wamekuwa wakimsubiri kwa muda wote huo ambao alikuwa kimya baada ya kuachia wimbo wake wa mwisho ambao bado unafanya poa mpaka sasa.

Mbali na hilo mkali huyo amewatahadharisha wasanii wenzake ambao walikuwa wakitamba katika soko la muziki muda ambao alikuwa kimya kuwa wakae sawa kwani muda wake kurudi na kufanya kazi umewadia, hivyo wanalazimika kumpisha maana amedai wamecheza sana na muziki.

"Nawashukuru sana wadau wangu wa kazi zangu...kazi inakuja kazi mpya kutoka kwa kijana wenu imefika takribani miaka mitatu sasa tangu nilipotoa wimbo wangu wa mwisho 'Pesa' ambao mpaka leo bado upo namshukuru muumba aliyenipa kipaji cha kutengeneza nyimbo zinazodumu, watoto wameshacheza sana muda wao wa kwenda kulala umefika nafikiri wote mnajua kuwa watoto wanatakiwa kulala mapema hasa baba anapokuwa amerudi," alisema Mr Blue.

Follow
Nawashuru sana wadau wangu wa kazi zangu...kazi inakuja kazi mpya kutoka kwa kijana wenu imefika takribani miaka mitatu sasa toka nilipotoa nyimbo yangu ya mwisho :"PESA":. ambayo mpaka leo bado ipo namshukuru muumba aliyenipa kipaji cha kutengeneza nyimbo zinazodumu ..watoto wameshacheza sana mda wao wa kwenda kulala umefika nafikiri wote mnajua kuwa watoto wanatakiwa kulala mapema hasa baba anapokuwa amerudi...nawapenda mashabiki zangu na napenda mnavyonivumilia...#onelov#
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment