NAPE-Lowassa Amepewa Hiyo Nafasi ya Kugombea Urais Baada ya Kuinunua Kwa Viongozi wa Ukawa



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema Lowassa hapendwi na wafuasi wa vyama vya upinzani, isipokuwa alipewa nafasi hiyo baada ya kuinunua kwa viongozi wa Ukawa, ambao wana tamaa ya fedha.
"Kila mtu anajua kuwa huyu bwana ameinunua hii nafasi kwa viongozi wa Ukawa, ndiyo maana watu wenye akili zao, wameamua kujiweka pembeni wamewaachia wenyewe na mzigo wao usiobebeka, inashangaza kuwa sisi tunawafukuza mafisadi wao wanawapokea, sasa wakipewa nchi si itakuwa hatari zaidi. Hivi umeshawasikia tangu ajiunge nao wanazungumza kuhusu ufisadi? Wanaona aibu kwa sababu katika nchi hii, ukitaja fisadi na mafisadi huwezi kumweka kando. Unafikiri Watanzania ni wajinga kiasi kwamba hawaoni huu usanii??” alihoji Nape.

Source GPL
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment