Nay wa Mitego afanya ngoma na Wizkid pamoja na Runtown wote kutoka Nigeria!


Ney wa Mitego kwa mara ya kwanza amefanya wimbo wa ushirikiano na wasanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria, huku nyimbo hizo akipanga kuziachia mwishoni mwa mwaka huu.


Ney aliliambia MTANZANIA kwamba, wasanii alioshirikiana nao ni mkali wa wimbo wa ‘Ojogduma’, Wizkid na Runtown ambao wote ni kutoka nchini Nigeria.

“Wimbo nilioshirikiana na msanii, Runtown nitautoa mwishoni mwa mwaka huu, lakini nilioshirikiana na Wizkid nitauachia mwakani kutokana na nilivyopanga mambo yangu,” alifafanua Ney.

Hata hivyo, mwanahip hop huyo kwa sasa anatarajia kuachia wimbo alioupa jina la ‘Nyumbani kwetu’, ambao hajamshirikisha msanii yeyote.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment