Belle 9 adai hawezi kumtumia mpenzi wake kama ‘kiki’ ya muziki
Belle 9 amedai kuwa sio vizuri msanii kumfanya mpenzi wake kiki ya muziki.
Belle amesema anashangazwa kuona wasanii wanawafanya wapenzi wao kama njia ya kujipatia umaarufu.
“Hiki kitu kimekuwa common sana,” amesema. “Wengine wanafanya kama kiki ya kufanyia biashara, mimi najua nafanya muziki lakini natokea pia kwenye mazingira ya dini. Familia ambayo ina maadili ya dini, sidhani kama kuna vitu watakuwa wanavifurahia kila wakati, sio kuongea kwa mambo yangu binafsi ndio niifanye kama ngao yangu kwenye muziki,” alisema.
“Mimi naamini muziki wangu, inamtosha kabisa mtu apate vitamin,” Belle aliambia Story Tatu ya Planet Bongo kupitia East Africa Radio.
0 comments:
Post a Comment