Ile kampeni waliyoianza Sauti Sol wa Kenya kwenye mitandao wa Instagram na Twitter, ya kuwashirikisha mashabiki wao kumshawishi staa wa R&B wa Marekani John Legend ashiriki kwenye remix ya single yao mpya ‘Isabella’, sio kitu cha siku moja wala mbili.
Kwa mujibu wa Publicists wa Sauti Sol, Anyiko PR, wameiambia Mpasho ya Kenya kuwa Sauti Sol wamedhamiria kufanya kampeni hiyo kwa siku 30.
Ameongeza kuwa hakuna mawasiliano yoyote rasmi ambayo yameshafanyika kati yao na John Legend kuhusu mpango wa kumshirikisha kwenye remix, bali wameamua kutumia kwanza njia hiyo ili mshindi huyo wa tuzo tisa za Grammy awafahamu Sauti Sol ni kina nani, na aujue wimbo wa Isabella kwa kutumia nguvu ya mashabiki.
Kupitia mitandao yao wamewaelekeza mashabiki jinsi ya kushiriki kwenye kampeni hiyo;
“If you’d like to see John Legend on the Isabella remix, all you have to do is on your twitter or Instagram, upload a screen shot of the Isabella lyric video or artwork and tag @johnlegend #JohnLegendforIsabellaRemix.”
0 comments:
Post a Comment