Bonge la Nyau amesema mama yake Matonya alishtuka baada ya kutambulishwa kwake mara ya kwanza.
“Nilikuwa naitwa Bonge la Nyau lakini sasa hivi Nyauloso,” aliimbia 255 ya XXL kwenye Clouds FM.
“Nimejiita Bonge la Nyau mimi lakini watu wengine hawapendi, wananiambia jina baya na mwonekano ni tofauti na jina. Juzi nilienda nyumbani kwa akina Matonya walitualika chakula, baada ya kumaliza chakula tukaanza kutambulishwa, wametambulishwa wengine baada ya kufika kwangu, akatambulisha ‘mama huyu anaitwa Bonge la Nyau’, akashtuka, akaanza kucheka! Akaniuliza ‘umefikiria nini mwanangu mpaka kujiita hivyo’, nikagundua ni kitu fulani kina sound kinatisha zaidi. Lakini sasa baada ya kujiita Nyauloso kila mtu amefurahia.”
0 comments:
Post a Comment