Rais wa Congo-Brazzaville ametangaza kuwa nchi hiyo itaandaa kura ya maamuzi kuamua iwapo taifa hilo litabadilisha katiba kumruhusu kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Rais Denis Sassou Nguesso ametoa tangazo hilo kwenye hotuba kupitia redio na runinga ya taifa.
Hata hivyo, hakutoa tarehe ya kufanyika kwa kura hiyo.
Rais huyo aliongoza Congo kuanzia 1979 hadi 1992 kipindi cha kwanza kabla ya kurejea mamlakani kwa kipindi cha sasa mwaka 1997.
Uganda na Burundi tayari zimewahi kubadilisha katiba kutoa fursa kwa marais walio mamlakani kuendelea kuongoza.
Nchini Rwanda, mjadala bado unaendelea kuhusu wazo la kubadilisha katiba kumruhusu Rais Paul Kagame kuwania tena urais.
0 comments:
Post a Comment