Davido asema hana mpango kabisa wa kuoa kwa sasa



Licha ya kujaliwa kupata mtoto wa kwanza mwaka huu, star wa Nigeria, Davido amesema hafikirii kabisa kuoa kwa sasa.

Davido akiwa na baby mama wake

Katika mahojiano na gazeti la Punch la Naija, star huyo ambaye wiki iliyopita ametoa wimbo mpya ‘Dodo’, alipoulizwa kama baada ya kujaliwa kupata mtoto kama anafikiria kuoa alijibu, “Sifikirii kabisa, sina mpango wa kuoa kwa sasa”.

Alipoulizwa swali lingine kama muda wa kuoa utakapofika endapo atamuoa mama wa mtoto wake au ana msichana mwingine aliyepanga kumuoa, Davido alikwepa kujibu alichoulizwa na badala yake akarudia jibu la mwanzo “sina mpango wa kuoa kwa sasa”.

Mwezi May mwaka huu David Adeleke a.k.a Davido (22) alifanikiwa kupata mtoto wa kike, na mama wa mtoto huyo anaitwa Sophie Momodu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment