Rapper Godzilla amewaunga mkono Weusi na wasanii wengine kwa kusema kuwa hawezi kufanya show za kisiasa ili kumsupport mgombea fulani.
Akizungumza kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Zizi alisema hawezi kuuza utu wake kwa pesa.
“Sasa hivi politics zimetawala, wasanii ni politics, mimi sio politics, siwezi kufanya hivyo na kitambulisho cha kura sasa sieliwi nampigia nani? Siwezi kufanya hivyo, siwezi kuuza utu wangu,” alisema Godzilla.
“Kwa mfano nakuita uje uni-promote halafu nakupa milioni 2, unaweza kutoka kwa milioni 2? Ukiwa na time table milioni 2 is just nothing.”
0 comments:
Post a Comment