Izzo Bizness aeleza kwanini wasanii wa Hip Hop wanakosa ‘management’ za kuwasimamia




Izzo B.psd_

Izzo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV kuwa wadau wengi waliona wasiwekeze pesa zao kwa wasanii wa Hip Hop wakiamini hazitarudi.

“Watu wengi wanaona wawekeze pesa yao mahali ambapo itarudi mapema na tangia mwanzo huu muziki wetu ulikuwa hauaminiki, watu wa kuimba wanaaminiwa sana, unaonekana ni muziki unaofika kote, tofauti na watu wa kurap,” alisema. “Historia huko nyuma inasema kulikuwa kuna ugomvi sana, kama unakumbuka kipindi cha nyuma watu walikuwa wanapigana, sasa ile hali ilikuwa inawatia watu mashaka, kwamba unaweza ukamfuata Izzo na kummanage, kaenda hewani ukizingua anakupiga roba,” alitania Izzo.

“Sasa hivi imeanza kuwa tofauti, ukizungumzia watu kama Weusi wana management yao, mtu kama AY ana uhakika, FA, imekuwa sasa management sio lazima aje mtu mwenye pesa nyingi awekeze. Mimi naweza hata mdogo wangu akawa amewekeza kwangu, as long as tunapata mawazo bora na mikakati bora. Hiyo ndio maana halisi ya management, sio kupewa pesa ukaimbe na kwenye nyimbo umtaje mtu, hapana maana ya management ni uongozi bora.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment