Rapper Izzo Bizness amesema anajipanga kuachia kazi yake mpya aliyowashirikisha Mwana FA pamoja na G-Nako.
Izzo ameiambia Story Tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa anajisikia faraja kufanya kazi na rapper kama FA ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki wake kwa nyakati tofauti.
“Ngoma yangu mpya nimewashirikisha G-Nako pamoja na Mwana FA na producer aliyengeneza beat ni Nahreel kutoka The Industry,” amesema. “Hii itakuwa ni project tofauti kwa sababu ni ngoma yangu ya kwanza kufanya kazi na Mwana FA, najua FA ni rapper mkubwa, rapper ninayemheshimu sana, rapper mwenye uwezo wa hali ya juu. Pia G-Nako ni chorus killer ambao tunao Tanzania, kwahiyo mashabiki wasubirie kitu kizuri kinakuja,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment