Jux: Jackie Cliff anajua nipo na Vanessa Mdee


Jux amedai kuwa Jackie Cliff (aliyekuwa girlfriend wake) aliyedaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China na kufungwa jela, anaendelea vizuri na anafuatilia kila kitu kinachoendelea Bongo.

jux na Jackie

Jux amesema Jackie anajua mahusiano yake na Vanessa Mdee.
“Yeah tunawasiliana tunaongea,” amesema Jux. “Anajua kila kitu kinachoendelea. Tunaongea vizuri, yuko poa kabisa na habari za Bongo kila kitu anajua yaani,” Jux alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa TV.
“Kuna habari nyingine hata mimi nashangaa anajuaje, kwa sababu kuna rafiki zake wengine wanaenda kumuona, pia mimi ni kijana I want to move on in my life, na yeye mwenyewe anajua inabidi niendelee na maisha, kikubwa zaidi tunawasiliana na hatuna mahusiano yoyote mabaya.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment