Black Rhino amekiambia kipindi cha Chill na Sky kuwa wimbo huo ulifanyika katika mazingira yenye ushindani mkubwa.
“Kila mtu alikuwa anataka amuonesha mwenzake kwamba, me I am the best, kwahiyo ilikuwa ni ushindani fulani,” anakumbushia Rhino.
“Huwezi amini kila mtu alikuwa anaandika mashairi kwake lakini alikuwa hayupo mwenzie anayejua kachana nini. Kwahiyo kila mtu alikuwa anamtegea mwenzake atasikia verse yangu tukiwa booth.”
Anasema hata siku wanaingia sauti Bongo Records walikuwa wanategeana baada ya Fid kuingiza sauti yake.
“Sasa ikawa akimaliza Fid nani aingie!, kati yangu mimi, Adili na Langa hapo ndipo ulikuwa mtihani sababu sisi ndio tulikuwa madogo kila mtu anamtolea macho mwenzie kwamba huyu asinifunike.”
Msikilize Blach Rhino akiongelea collabo hiyo.
0 comments:
Post a Comment