Kanisa Katoliki Laja na Mpya..Sasa Kama Upo Kwenye Ndoa Unaweza Mpa Mwenzako Talaka..Kama Wafanyavyo Waislam





KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.

Dhamira hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Papa huyo kutaka kulifanya Kanisa Katoliki liwe rafiki zaidi na kuendana matakwa ya walio wengi.

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Papa alisema si haki kwa wenzi kuishi muda mrefu ‘wakikandamizwa na wingu la shaka’ kuhusu uhalali wa ndoa zao.

Ikumbukwe kwamba ni msimamo wa Papa kumkatalia Mfalme Henry the VIII wa Uingereza kumtaliki mkewe Catherine wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha England ijitenge na Rome na kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England huku mfalme akiwa mlinzi wa Imani wa kanisa hilo.

Mabadiliko makuu matatu aliyotangaza Papa jana ni kuondoa mchakato wa mapitio ya mara ya pili wa uamuzi wa kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa kabla ya ndoa kuvunjwa.

Mengine ni kuwapatia maaskofu uwezo wa kuharakisha na kuvunja ndoa wenzi wanapoamua wenyewe katika mazingira fulani kama vile ukatili katika ndoa au uasherati na mchakato huo wa talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa ada ndogo kwa ajili ya gharama za utawala.

Kabla ya sheria hiyo, Wakatoliki waliotaka talaka walihitaji kibali kutoka kwa mahakama mbili za kanisa, wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa rufaa bado zinaruhusiwa.

Kabla ya sheria hiyo, wanandoa wa Wakatoliki wanaotalikiana bila idhini ya kanisa na kuolewa upya walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa kupokea komunio.

Lakini kwa mujibu wa utaratibu mpya, wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi wa kanisa hilo.

Mwaka jana Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa hilo kuboresha na kurekebisha taratibu hizo kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza gharama.

Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili zinazoitwa ‘motu proprio’, neno la kilatini lililobuniwa na Papa mwenyewe.

Taratibu hizo zitakuwa rasmi kama sehemu ya sheria za kanisa (canon law) ifikapo Desemba 8 mwaka huu wakati Papa atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee ambao kwa kawaida huhusishwa na msamaha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment