Mchezaji wa Yanga Canavaro Kuchukuliwa Hatua za Kinidhamu Baada ya Kupiga Picha na Jezi ya Yanga Kuonyesha Akimsupport Magufuli






Headlines za uchaguzi mkuu 2015 bado zinazidi kuchukua nafasi, tumekuwa tukiona watu maarufu kama wasanii wa filamu na Bongofleva wakionyesha hisia zao kwa wagombea wawapendao. Ila kwa wachezaji mpira wa miguu ni tofauti kidogo kulingana na sheria za vilabu vyao pamoja na mikataba yao.

Baada ya kuonekana kwa picha ya nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro akimsuport moja kati ya wagombea Urais wa mwaka 2015, kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na sheria ya wachezaji kuonesha hisia zao kwa vyama wavipendavyo hususani wakiwa wamevaa jezi za vilabu vyao.

katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha Kazungumza kuhusiana na Cannavaro kuvaa jezi za Yanga na kupiga picha akionyesha hisia zake kwa mgombea huyo.

“Mimi nafikiri Cannavaro angekwenda akiwa amevaa nguo zake za kawaida na kuonyesha kumsuport Magufuli au mwingine isingekuwa na tatizo. Sisi tunachozungumzia ni yeye kuvaa jezi ya klabu na yenye nembo ya mdhamini wetu halafu unaonyesha kushabikia siasa, Cannavaro amekosea hivyo kama klabu tumekaa chini na tutaangalia hatua za kinidhamu zipi zichukuliwe”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment