Meneja wa Q-Chief na MB Dog adai ameshatumia zaidi ya mil 300 kwa wasanii hao


Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment inayowasimamia Q-Chief, MB Dog na wasanii wengine imedai hadi sasa imetumia zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wasanii wake katika kipindi cha miaka minne.

11084803_454426184708830_584710411_n

Mkuregenzi wa kampuni hiyo, J. Mhonda amesema licha ya kutumia gharama hiyo mpaka sasa hategemei kama itarudi.
“Kampuni nimeianzisha ndani ya miaka 4 iliyopita, ndani ya miaka 4 kwa haraka haraka ni pesa nyingi sana [imetumika]. Kwanza niliwanunulia magari na ni magari ambayo mtu anaenda kuchukua show room, gari milioni 20 na kitu kwa baadhi ya wasanii,” Mhonda aliiambia XXL ya Clouds FM.
“Halafu uje uingize gharama ya kufanya video za wasanii mbalimbali, kama Q Chillah tumeshafanya video tatu Afrika Kusini pamoja na wasanii wengine. Yaani nimeshatumia zaidi ya milioni 300 na kuendelea. Bado haijarudi hata kidogo,” aliongeza.
“Kwangu mimi sichukulii kama hasara. Muziki ni kama sehemu ya maisha yangu ndio maana naendelea kusupport.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment