Milipuko ya mabomu yaua watu 20 Syria



Mji wa Hassakeh umekuwa ukishuhudia mapigano makali
Watu 20 wamefariki kwenye milipuko miwili ya mabomu ya kutegwa kwenye magari katika mji wa Hassakeh nchini Syria.

Kituo cha runinga cha serikali nchini humo kimesema watu 40 wamejeruhiwa.

Shambulio moja lililenga vikosi vya Kikurdi, kwa mujibu wa shirika moja ya kutetea haki lenye makao yake Uingereza.

Runinga ya taifa nchini humo ilionyesha kanda ya video ya nyumba zilizoharibiwa vibaya kwenye mashambulio hayo.

Baadhi ya maeneo katika mji huo yanadhibitiwa na wanajeshi wa serikali na mengine wapiganaji wa Kikurdi, lakini wapiganaji wa Islamic State wamekuwa wakijaribu kuutwaa pia.

Kituo hicho cha televisheni kilisema waokoaji wanasaka miili na manusura kwenye vifusi.

Mwezi Juni, Umoja wa Mataifa ulisema takriban watu 50,000 wametoroka makwao Hassakeh baada ya wapiganaji wa IS kuvamia eneo hilo. Wengine 10,000 walitorokea kaskazini kuelekea mpaka wa taifa hilo la Uturuki.

Watu 200,000 wameuawa na wengine 11 milioni kutoroka makwao nchini Syria kufuatia mapigano yaliyodumu miaka minne sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment