Msanii wa Nigeria, Runtown ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye fainali za shindano la Bongo Star Search, imefahamika.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production na ambaye pia ni jaji mkuu wa shindano hilo, Rita Paulsen alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki kwenye Instagram Jumatano hii.
Madam Rita amedai kuwa pamoja na Runtown anayetamba kwa sasa na wimbo wake ‘Banger’ alioshirikiana na Uhuru, wasanii wengine watakaopanda jukwaani kutumbuiza ni Christian Bella, Yamoto Band, Navy Kenzo, Peter Msechu na Kala Jeremiah.
Runtown amewahi kuonesha nia ya kuurudia wimbo ‘Wanjera’ wa Ommy Dimpoz.
Fainali za shindano hilo zitafanyika Ijumaa ya October 9 kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment