Ommy Dimpoz amesimulia namna alivyoingizwa mjini kwa kuibiwa simu yake ya mkononi akiwa dukani jimboni Texas nchini Marekani alikokwenda kwa ziara ya kimuziki.
Dimpoz ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa baada ya kufanya show ya kwanza aliamua kufanya ‘shopping’ kwenye duka moja kubwa la nguo mjini Houston, lakini baada ya muda akajikuta hana simu.
“Niliangalia mfukoni sikuikuta, nikajaribu kuipiga haikuita nilipomwambia mwenye duka akanipeleka katika kamera za usalama ndani ya duka hilo nikamuona mwizi wa simu yangu alikuwa mmoja wa wateja katika duka hilo,” alieleza Dimpoz.
Pia Ommy alisema simu hiyo ilikuwa na hifadhi ya nyimbo zake mpya ambazo hakutarajia kuzitoa kwa sasa na vitu vingine binafsi vingi jambo ambalo limemtia hasara kubwa.
0 comments:
Post a Comment